Jumatano 6 Mei 2026 - 20:38
Kufikisha ujumbe wa dini kupitia tabia na vitendo ni muhimu zaidi kuliko hotuba

Hawza/ Kongamano la tatu la “Kamati ya Malezi na Ulinganiaji” kwa uwepo wa Ibrahim Zakzaky nchini Nigeria lilihitimisha shughuli zake.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Sayyid Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, katika hotuba yake kwenye hafla ya kufunga mkutano wa Kamati ya Malezi na Ulinganiaji, alisisitiza umuhimu wa kufikisha ujumbe wa dini na akasema: Kufikisha ujumbe huu ambao waliutanguliza waliotangulia ndiko kulikoifanya dini idumu hadi leo. Hivyo basi, kufikisha ujumbe wa dini ni jukumu linaloendelea juu ya kila Muislamu hadi mwisho wa maisha yake.

Sheikh Zakzaky aliongeza: “Kama ambavyo Hussein ibn Ali (as) hadi dakika za mwisho za maisha yake alikuwa akiwahubiria wauaji wake, kwa njia hiyo hiyo dini itahifadhiwa na kupitishwa kwa vizazi vijavyo.”

Wakati huo huo, alisisitiza umuhimu wa ulinganiaji kupitia matendo mema na akasema: “Kufikisha ujumbe kwa njia ya vitendo ni muhimu zaidi kuliko kuufikisha kwa sauti na maneno.”

Katika muendelezo wa hotuba yake, alitahadhatisha kwamba; ni lazima kukabiliana na mitihani na shinikizo kutoka kwa watawala na wafuasi wao, kama ilivyokuwa katika historia yote. Hata hivyo, hatimaye Waumini watashinda, kama alivyoahidi Mwenyezi Mungu.

Mwishoni, kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alisisitiza umuhimu wa kuwalingania watu kwa hekima na kwa njia nzuri inayosaidia wao kuelewa vyema, pamoja na kujiepusha na mbinu kali na zisizofaa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha